Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda limepitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2019/2020 ambapo Halmashauri imekisia kukusanya jumla ya Tshs. 20,668,670,800.00 kati yake Tshs.1,869,216,000.00 ni kutoka vyanzo vyake vya Mapato ya Ndani, Tshs. 20,578,330,623.00 ni kutoka ruzuku ya Serikali kuu na Wafadhili.
Halmashauri inatarajia kukusanya jumla ya Tshs 1,869,216,000.00 kutokana na makusanyo yake Ndani kutoka vyanzo mbalimbali. Aidha makisio ya Mapato ya Ndani yamepungua kutoka Tshs. 2,442,436,000.00 kwa mwaka 2018/2019 kwenda Tshs. 1,869,216,000.00 kwa mwaka 2019/2020 sawa na punguzo la Tshs.573,220,000.00 ambayo ni 23.47%. kupungua kwa kadirio la Mapato kumetokana hasa na mabadiliko ya kisera ambapo baadhi ya vyanzo vya Mapato ya Ndani ya Halmashauri kuhamishiwa Serikali kuu na baadhi ya viwango vya tozo za ushuru kupunguzwa hasa tozo zitokanazo na ushuru wa Mazao.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.