Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mama Lilian C. Matinga ameliomba Baraza la Madiwani la Manispaa ya Mpanda kumuunga mkono kuwakataa waalimu wasiokuwa na maadili ambao wanawatongoza wanafunzi wao.
Ombi hilo limetotewa mapema leo wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.
Mama Matinga aliendelea kueleza kuwa, waalimu ni wazazi, hivyo kitendo cha kumtongoza mwanafunzi ni kinyume kabisa na maadili ya kazi, hivyo amewatahadharisha waaalimu kuwa, yeyote atakaye bainika au kukisia kuwa anapoteza ndoto za wanafunzi atachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Aidha aliendelea kuwasihi madiwani ili suala hilo lipewe kipaumbele kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa Mkoa wa Katavi ni kinara kwa mimba za utotoni. Hivyo amewataka madiwani kama wazazi, wananchi wote na jamii nzima kila mmoja kusimama kwa zamu yake na kutekeleza yale anayotakiwa kufanya. Amewataka madiwani kutekeleza wajibu wao.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.