Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mheshimiwa Jamila Yusuph ameongoza zoezi la upandaji miti Katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda,ikiwa ni hatua ya kuimarisha utunzaji wa Mazingira na kuimarisha ushirikiano wa jamii katika uhifadhi wa Rasilimali asilia.
Zoezi Hilo kimefanyika leo Tarehe 27 Januari 2026,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kulinda mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Aidha upandaji wa huo wa miti umefanyika kwa pamoja na kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais Samia,ambapo zoezi hilo limechukuliwa kama ishara ya heshima,Mshikamano, uzalendo na upendo.
"UZALENDO NI KUTUNZA MAZINGIRA SHIRIKI KUPANDA MITI".
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.