RAS KATAVI AKAGUA UKARABATI WA HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA
Katibu tawala mkoa wa Katavi ndugu Hassan Abbas Rugwa mapema leo tarehe 15 Aprili, 2023 amefanya ziara katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ili kujionea hatua za ukarabati na majengo mbalimbali unafanyika katika hospitali hiyo.
Akiwasilisha taarifa kwa katibu tawala Dk. Paul Swakala Mganga mkuu wa Manispaa ya Mpanda kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa alieleza kuwa, Mwezi desemba 2022 Manispaa ya Mpanda ilipokea fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda. Ukarabati ulianza mwezi februari ambapo jumla ya majengo 7 na njia za watembea kwa miguu yameanza kufanyiwa ukarabati. Aidha kupitia kiasi cha fedha kilichopokelewa pamoja na ukarabati manispaa inajenga Majengo mapya 3 ambayo ni jengo la mionzi (Radiology), jengo la upasuaji pamoja na kichomea taka.
Mganga mkuu aliendelea kueleza kuwa ukarabati pamoja na ujenzi unaendelea vizuri na kwamba mafundi wapo kazini na vifaa vilivyovingi vimenunuliwa, aidha mradi unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Juni 2023.
Kwa upande wake katibu tawala wa mkaoa wa Katavi ndugu Hassan Abbas Rugwa amefurahishwa na hatua za ukarabati pamoja na ujenzi unaoendelea, aidha ameridhishwa na viwango vya ubora katika ujenzi huo na kwamba kupitia shughuli zinazoendelea kufanyika anaiona thamani ya fedha.
Pia ameutaka uongozi wa hospital kuwa na mpando endelevu wa matumizi ya ardhi katika eneo la hospitali kwa kuwa hospitali hiyo ipo mjini na kwamba ipo siku Manispaa hii itakuwa Jiji.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.