RC KATAVI AZINDUA MITAMBO YA UCHIMBAJI WA VISIMA
Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka miwili madarakani imetoa zaidi ya shilingi bilioni 27.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 40 ya maji mkoani Katavi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko wakati akizindua mitambo ya uchimbaji visima.
RC Mrindoko amesema hadi sasa miradi 15 imekamilika na tayari Wananchi wanapata huduma huku miradi 25 ikiwa katika hatua ya ukamilishaji.
Aidha, amewataka Wananchi mkoani Katavi kuvitunza vyanzo vya maji sanjari na kuitunza miradi ya maji inayotekelezwa katika mkoa huo ili iwanufaishe kwa kuondokana na kero ya maji.
Amesema, hakutakuwa na maana Serikali kutoa mabilioni hayo ya fedha na mitambo kama vyanzo vya maji havitatunzwa.
"Niwaombe Wananchi wa Katavi, tunapo kwambia ondoka kwenye chanzo cha maji, ondoka kwenye msitu ambao tunautegemea fanya hivyo bila kujiuliza mara mbili"
Awali akitoa taarifa ya mitambo hiyo, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Katavi Mhandisi Peter Ngunula amesema, ujio wa mitambo hiyo itaongeza kasi ya usambazaji maji mkoani humo.
Ameongeza kuwa, kabla ya Mwaka 2025 wanauhakika upatikanaji wa maji utakuwa zaidi ya asilimia 85 kwani mitambo hiyo inauwezo wa kuchimba kisima hadi cha urefu wa mita 400 tofauti na awali walipolazimika kuchimba kisima cha urefu kama huo kwa kutumia mtambo zaidi ya mmoja.
RUWASA Mkoa wa Katavi inahudumia vijiji 172 ambapo kati ya vijiji hivyo, ni vijiji saba pekee bado havijafikiwa na huduma ya maji ambavyo hata hivyo tayari vipo kwenye bajeti.

Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.