RC KATAVI: SITAKI UNYANYASAJI SEHEMU ZA KAZI
Mkuu wa mkoa wa Katavi mhe. Mwananmvua mrindoko amewataka waajiri wote mkoani Katavi wa sekta binafsi na serikali kuto wanyanyasa wafanyakazi wao. Mhe. Mrindoko ameyasema hayo katika hafla ya siku ya wafanyakazi duniani ambapo kimkoa hafla hiyo imefanyika MANISPAA YA Mpanda viwanja vya shule ya msingi kashaulili.
Mhe mrindiko ameeleza kuwa Karibu miongo 6 ya uhuru wetu kama taifa, Tanzania tumepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kutokana na kufanya kazi. “Tuna vituo vingi vya kutolea afya, tuna dawa na vifaa tiba katika hospitali zetu, tuna mtandao mkubwa wa barabara, madaraja, viwanja vya ndege na bandari, tuna miundombinu ya elimu na vifaa mbali mbali vya kufundishia katika shule zetu. Tuna mambo mengi ya kimaendeleo katika nchi yetu”
Katika Mkoa wa Katavi tunajivunia maendeleo lukuki. Kwa kutaja machache, tuna hospitali na vituo vya kutolea huduma ya afya kwa wananchi wetu, tuna bandari, tuna kiwanja cha ndege, tuna barabara na bandari, tuna chakula cha kutosha kwa wananchi wetu” Alisema Mrindoko.
Bidii na maarifa ya kazi kwa wafanyakazi wa umma, sekta binafsi kwa kushirikiana na wananchi wa Mkoa wa Katavi umepata maendeleo makubwa katika sekta mbali mbali.
Katika maadhimisho ya kumbukizi ya Siku ya wafanyakazi duniani, yaliyoadhimishwa kimkoa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili, Mjini Mpanda, Kiongozi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko, kwa dhati ya moyo wake, hakusta kuwapongeza wafanyakazi wote katika mkoa wake kwa kazi nzuri waliyofanya katika kuwahudumia wananchi wa mkoa huo.
Mhe. Mrindoko amewataarifu wafanyakazi kuwa kazi wanazozifanya katika mkoa wake ndizo ambazo zimeleta mafanikio makubwa na kuuheshimisha mkoa.
Amebainisha kazi hizo kuwa ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM, utoaji wa huduma na utatuzi wa kero mbali mbali kwa wananchi.
Kiongozi huyo, amewasihi wanafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa, nidhamu ya hali ya juu, kujituma na kutumia muda wao vizuri katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa mkoa wake.
Amewaahidi wafanyakazi hao kuwa serikali ya mkoa wake itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kazi kwa wafanyakazi wote ili kuwezesha mipango, programu na miradi ya maendeleo kusonga mbele zaidi.
Amewaonya waajiri wote katika mkoa wake kutojihusisha na unyanyasaji wa wafanyakzi wao, kudumisha staha sehemu za kazi, nidhamu na kuwathamini na kuwaheshimu wafanyakazi wote kwa mujibu wa Sheria, Kanununi, Taratibu, Miongozo, Mila na Desturi za kitanzania.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.