Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwanamvua Mrindoko, Leo Januari 28,2026 ameongoza zoezi la upandaji miti Katika Shule ya Sekondari Kishaki iliyopo Manispaa ya Mpanda ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha utunzaji wa Mazingira.
Akizungumza amempongeza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake thabiti na dira madhubuti ya kuhakikisha masuala ya utunzaji wa Mazingira yanapewa kipaumbele cha juu Kitaifa.
Aidha Mrindoko amewasisitiza wananchi pamoja na wadau wote wa Maendeleo kuitunza miti inayoendelea kupandwa ili kuhakikisha Mkoa wa Katavi unakuwa na mazingira rafiki muda wote.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.