Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, ameungana na mamia ya waumini na wakazi wa mkoa wa Katavi katika mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa kiroho wa Kanisa la New Harvest Church marahemu Askofu Dkt. Laban Ndimubenya. Mazishi hayo yamefanyika katika Kanisa la New Harvest Church, yaliyofanyika februari 9, 2025 Mikocheni, Manispaa ya Mpanda yakiambatana na majonzi makubwa kutoka kwa waombolezaji mbalimbali kutoka ndani ya nchi nan je ya nchi.
“Kifo cha Askofu Dkt. Laban ni pigo kubwa kwa Taifa, si kwa Kanisa pekee, kwani marehemu alikuwa mwalimu wa maadili mema, mshauri wa jamii, na kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo” alisema Mwanamvua mrindoko Mkuu wa mkoa wa katavi.
Mhe. Mrindoko aliwaeleza waombolezaji kuwa,Tumepoteza mtu wa pekee, mtu wa hekima na busara, aliyejitolea kwa dhati kuhudumia jamii kwa moyo wa upendo na kwamba Mchango wake haukuwa tu katika uwanja wa kiroho bali pia katika sekta za elimu, afya, na ustawi wa jamii. Alikuwa nguzo muhimu ya maendeleo katika mkoa huu wa Katavi na nchi kwa ujumla," amesema RC Mrindoko huku akitoa pole kwa familia, waumini, na wote walioguswa na msiba huo.
RC Mrindoko ameongeza kuwa Serikali itaendelea kumuenzi Askofu Dkt. Laban kwa kuthamini mchango wake na kuendeleza juhudi alizozianzisha katika sekta mbalimbali.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.