WAFANYABIASHARA WA MAZAO NA WENYE MAGHALA KUSAJILIWA KIDIGITALI
Mkuu wa wilaya ya Mpanda mhe Jamila Yusuph amewataka Wafanyabiashara wa mazoa waliopo wilaya ya mpanda kutoa ushirikaiano kwa maafisa wa Serikali watakaopita kwenye biashara zao ili kutekeleza zoezi la usajili wa biashara ikiwa ni utekelezaji wa zoezi la urasimishaji wa biashara zao ili kuendana na na matakwa ya Wizara ya Kilimo ambayo yanamtaka kila mfanyabishara wa mazoa kurasimiasha biasahara yake.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya mapema leo Julai 6, 2023 katika kikao chake na wafanyabiashara kilichofanyika katika ukumbi wa Manispa ya Mpanda kikiwa na lengo la kuwaeleza zoezi la Urasimishaji wa Biashara ya mazao ya Kilimo kwa kuboresha utaratibu wa Uuzaji na Ununuzi wa Mazao ya Kilimo nchini ambapo utaratibu huo unasimamiwa na Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha Mhe Jamila elmeeleza kuwa Lengo serikali la kuboresha Utaratibu huu ni pamoja na Kuwalinda wakulima na wafanyabiashara dhidi ya usumbufu na utapeli unaotokea katika biashara ya mazao ya kilimo, Kurasimisha Sekta ya Kilimo Mazao ili kuwezesha ufanyaji biashara kwa mujibu wa sheria na taratibu, Kuwalinda wafanyabiashara wa ndani dhidi ya wafanyabiashara kutoka nje ya Tanzania wanaonunua mazao moja kwa moja shambani, Kuwasaidia wakulima wa Tanzania kunufaika kutokana na jitihada za Serikali za kutoa ruzuku na uwekezaji unaoendelea ili kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji Pamoja na Kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za biashara ya mazao ya kilimo ikiwa ni pamoja na kujua hali halisi ya usalama wa chakula nchini.
Mhe Jamila ameeleza kuwa Ili serikali iweze kutimiza malengo iliyojiwekea na ili wafanyabiashara waweze kuuza au kununua mazao katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wanatakiwa fanya mambo yafuatayo:
Wafanyabiashara wote wa Mazao ya Kilimo ni lazima “Wanunulie na Kuuzia” Mazao yao kwenye Vituo maalum Vilivyoainishwa na si vinginevyo.
Wafanyabiashara wote wahakikishe wanatumia Mizani katika Kununua Mazao ya Kilimo. Aidha Mizani hizo ni lazima ziwe zimethibitishwa ubora na Wakala wa Vipimo.
Wafanyabiashara wote wa mazao ya kilimo ni Lazima wasajiliwe na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ili kuwatambua na pia kuwa na Takwimu sahihi za Mazao yote yaliyouzwa na kununuliwa kupitia wao. Aidha hakuna gharama yoyote ya Kusajili “NI BURE”.
Wanunuzi wa mazao kutoka nje ya nchi Ni lazima wanunue Mazao yao kupitia kwa wafanyabiashara wa mazao ya kilimo waliosajiliwa Manispaa na siyo kununua mashambani. Aidha Mfanyabiashara yeyote wa Kigeni akikamatwa ananunua Mazao Kijijini kwa Wakulima, Hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Ghala zote zinazohifadhi mazao ya kilimo nchini (binafsi, ushirika, Serikali) zitasajiliwa kupitia mfumo wa Kielektroniki na kupatiwa namba maalumu ya utambulisho bila gharama yoyote. Aidha, kila mfanyabiashara wa mazao ya kilimo hapa nchini atalazimika kutoa taarifa ya kiasi cha mazao yaliyonunuliwa, yaliyohifadhiwa na kuuzwa kupitia mfumo huo
Mfanyabiashara anayesafirisha mazao ya kilimo ndani ya nchi atapaswa kupata kibali cha kusafirisha mazao (movement order) kutoka ofisi za wakuu wa Wilaya husika. Kibali hicho kitawawezesha wafanyabiashara kusafirisha mazao kutoka Wilaya moja kwenda nyingine na kutoka Mkoa mmoja kwenda mwingine; Kibali kitatolewa Bure Kabisa.
Wafanyabiashara wote wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutumia madalali wakati wa kuomba vibali vya kusafirisha mazao ya kilimo nje ya nchi, bali waombe moja kwa moja kupitia mfumo wa ATMIS au kufika kwenye Ofisi za Wizara ya Kilimo kwa msaada zaidi; na
Wafanyabiashara wa mazao ya kilimo wenye Mikataba maalum ya kununua mazao kwa wakulima Ni lazima wawasilishe nakala za mikataba hiyo Ofisi za Manispaa ya Mpanda kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.
Akizungumza mbela ya Mkuu wa Wilaya Ally Seif ambaye ni mfanyabiasha wa mazao na mmiliki wa ghala kwa niaba ya wafanyabiasha ameishukuru serikali kwa kuanzisha utaratibu huu wenye lengo la kumlinda mkulima na mfanyabiashara wa ndani. Amewasihi wafanyabiashara wenzake kulipokea zoezi hilo kwa mtazamo Chanya na kuwataka kwenda kwenye utekelezaji.
Aidha wafanyabiashara wamemuomba Mkuu wa wilaya baada ya mwezi mmoja wa utekelezaji aitishe kikao cha tathimini ili kuona na kutatua changamoto zitakazokuwa zimejitokeza wakati wa utekelezaji jambo ambalo lilikubaliwa na mkuu wa wilaya ambapo kikao cha tathimini kitafanyika Agosti 15, 2023.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.