Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bi, Marietha Mlozi amewataka Wajasiriamali wanaofanya shughuli zao katika stendi ya ya mabasi ya Mizengo Pinda kuunda vikundi kazi ili kuweza kukutana na fursa zinazo weza kujitokeza mbele ikiwa ni pamoja kutambulika na kupata elimu mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano wake uliofanyika katika eneo la Stendi kuu ya Mabasi Mizengo Pinda katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Amewataka wajasiriamali hao kujikita katika kujikwamua kiuchumi na kuwa na tabia ya kujiwekeza.
Aidha Bi, Jeni Lwakabamba ambaye ni mratibu uwezeshaji Wananchi kiuchumi amesema Halmashauri Manispaa ya Mpanda inatalajia kutoa Mikopo zaidi ya Millioni 250 ikiwa ni bajeti ya asilimia kumi ya Mapato ya ndani mbali na mfuko wa Marejesho ya mikopo ya vikundi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.