TANGAZO TANGAZO
MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA KWA MWAKA 2017 UTAFANYIKA KATIKA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI TAREHE 2/04 KATIKA UWANJA WA MWENGE ULIOPO KASIMBA KATA YA ILEMBO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA ITAUPOKEA MWENGE WA UHURU SIKU YA JUMAPILI TAREHE 02/04/2017 SAA 1:00 ASUBUHI KATIKA UWANJA WA MWENGE ULIOPO KASIMBA KATA YA ILEMBO NYUMA YA OFISI YA MKUU WA MKOA.
BAADA YA MAPOKEZI HAYO MWENGE UTAKIMBIZWA KUTEMBELELEA MIRADI NA VIKUNDI MBALIMBALI KATIKA KATA ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA
HIVYO WANANCHI WOTE MNATAKIWA KUFIKA KATIKA UWANJA WA MWENGE SAA 1:00 ASUBUHI KWA AJIRI YA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU.
AIDHA WANANCHI WOTE MNATAKIWA KUFIKA KWENYE VIKUNDI/MIRADI YOTE AMBAYO ITATEMBELEWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU.
PIA WANANCHI WOTE MNAOMBWA KUSHIRIKI KWA KUUKIMBIZA MWENGE WA UHURU KWA MWAKA 2017 WENYE KAULI MBIU YA “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU”
ATAKAYESIKIA TANGAZO HILI AMTAARIFU NA MWENZAKE.
Imetolewa na:
Albert Kyando
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa Ya Mpanda
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.