SERIKALI YALETA BILIONI 29 MANISPAA YA MPANDA NDANI YA MIAKA 5
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Mpanda Mhe. Haidary Sumry amesema serikali kwa kipindi cha miaka Mitano kuanzia Mwaka 2020/2025 imeleta fedha kiasi zaidi Bilioni 29 kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akitoa taarifa kwa wandishi wa Habari Mkoa wa Katavi Sumry amesema kuwa kwa kipindi cha Miaka mitano katika Manispaa ya Mpanda kumekuwa na mwendelezo wa kuleta fedha za miradi ya maendeleo kwa kiwango kikubwa hali ambayo imepelekea kuimarika kwa huduma za wananchi kupitia fedha za maendeleo.
Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi kupitia sekta ya Elimu,Afya,miundombinu na Maji kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wanachi.
Katika sekta ya Elimu Msingi kwa kipindi cha Miaka Mitano iliyopita kupitia fedha mbalimbali za serikali Manispaa ya Mpanda imefanikiwa kujenga Shule za Msingi mpya tano zenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5 kwenye shule hizo tano Halmashauri imefanikiwa kujenga Shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza.
Kuhusu ujenzi wa Madarasa kwenye Elimu ya Msingi Sumry ameeleza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 128 vye thamani ya shilingi bilioni 3.6
Kwenye eneo la miundombinu ya Madarasa kwa kipindi cha Miaka mitano Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika kukabiliana na upungufu wa Madawati kwenye eneo la Elimu Msingi Manispaa ya Mpanda imefanikiwa kutengeneza madawati 3310 pamoja na kujenga matundu ya vyoo 154 yenye thamani ya Shilingi Milioni 180.
Katika upande wa Elimu Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imefanikiwa kujenga Sekondari Mpya Katika Kata ya Mwamkulu,na Nsemlwa pamoja na kuongeza Sekondari mpya za sekondari kwenye baadhi ya kata ikiwemo Kata ya Kazima,na Kata ya Shanwe pamoja na Kata ya Nsemlwa.
‘’Kwahiyo kama Manispaa kwa kipindi cha miaka mitano tumefanikiwa kujenga Sekondari mpya Nane zenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.1’’ anasema Sumry .
Katika eneo la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye Elimu Sekondari amesema kuwa wamefanikiwa kujenga vyumba vya Madarasa 55 yenye thamani ya Shilingi Bilioni1.2 pamoja na kutengeneza viti na meza 2160 zenye thamani ya shilingi Milioni 151.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika eneo hilo la Ellimu ya Sekondari imefanikiwa kujenga matundu ya vyoo 38 kwa gharama ya shilingi Milioni 75 pamoja na kufanikiwa kujenga Mabweni Nane kwa Gharama ya shilingi Milioni 827.
Katika eneo la Sekta ya Afya Mstahiki Meya Sumry amesema kwa kipindi cha miaka mitano wameweza kufanya ukarabati wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa Gharama ya Milioni 900 huku wakifanikiwa kujenga vituo vya afya vitatu vyenye Thamani ya Shilingi Bilioni 1.5 huku kituo kimoja kipombioni kuanza kujengwa Kata ya Misunkumilo.
Kuhusu ujenzi wa Zahanati amesema Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imefanikiwa kujenga Zahanati tano zenye thamani ya shilingi milioni 560.
Katika Sekta ya Kilimo Sumry ameipongeza serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuimarisha sekta ya Hususani eneo la Kilimo cha umwagiliaji ambapo kwa kipindi cha miaka mitano Manispaa ya Mpanda imefanikiwa kupata mradi wa kilimo cha umwagiliaji kata ya mwamkulu wenye thamani ya shilingi Bilioni 31 ambao unaendelea kujengwa.
Amesema kuwa kwa namna ya pekee anamshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kiasi hicho cha fedha cha Zaidi ya Bilioni 29 kuzileta Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi kwaajili ya kusaidia kutatua kero za wananchi kupitia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.