MADIWANI WAAGA RASMI
Baraza la Madiwani la halmashauri ya Manispaa ya Mpanda leo Juni 19,2025 limeaga rasimi na kueleza utekelezaji wa miradi ya Maendeleo katika kila Kata.
Akihitimisha Baraza hilo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry amesema utekelezaji na mafanikio mbalimbali ya ujenzi wa miradi na utoaji wa huduma kwa Wananchi wa Manispaa hiyo kumetokana na ushirikiano wa Madiwani hao, watendaji wa Halmashauri chini ya Mkurugenzi Sofia Kumbuli , Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao Muda wote wamekuwa imara kuhakikisha Irani ya Uchaguzi inatekelezwa Ipasavyo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf ambaye alikuwa Mgeni rasimi ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta zaidi ya billion 200 kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo chini ya usimamizi wa madiwani imetekelezwa kwa ufanisi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.