JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MANISPAA YA MPANDA
|
TANGAZO
UHESABUJI WA MALI ZA HALMASHAURI YA MANISPAA MPANDA KWA MWAKA WA FEDHA UNAOISHIA JUNI 30, 2018
29/05/2018
Halmashauri ya Manispaa Mpanda inapenda kuwatangazia wananchi wote wa Tanzania kwamba iko katika maandalizi ya ufugaji wake wa Mahesabu kwa mwaka wa fedha unaishia Jun 30,2018. Katika maandalizi hayo itakuwa kwenye zoezi la uhesabuji mali zake zote. Zoezi hilo litaanza tarehe 01/06/2018 hadi tarehe 30/06/2018, hivyo basi wakati wa zoezi hilo Halmashauri itasitisha baadhi ya huduma za uagizaji, upokeaji na utoaji wa mali kwa kipindi hiki cha zoezi la uhesabuji mali.
Zoezi hili litahusisha Makao Makuu ya Halmashauri na Idara zake, Ofisi za Kata na Mitaa, Vituo vya Afya, Zahanati, Shule za sekondari na Msingi.
Halmashauri ya Manispaa Mpanda inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki cha zoezi la uhesabuji mali za Halmashauri.
Natanguliza shukrani
Michael F. Nzyungu
Mkurugenzi wa Manispaa
MPANDA
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.