“Mimi sio mtu wa kusifia sifia lakini kwa hili naomba niseme, stendi hii ni moja kati ya stendi bora kabisa Tanzania. Ujenzi wake ni wa viwango, mimi binafsi nimeridhishwa sana na ukamilishaji wa stendi hii, nawapongeza sana viongozi wote kwa usimamizi mzuri” alisema Waziri Jaffo.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa stendi hiyo mratibu wa Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia Bi Mery Kanumba kwa niaba ya Mkurugenzi alieleza kuwa, Mradi huo Umetekelezwa kwa gharama za Tshs, 3,780,614,501.00 kati ya fedha hizo Tshs, 3,451,328,501 ni fedha za ujenzi na Tshs, 329,286,000.00 ni fedha kwa ajili ya malipo ya Mtaalamu Mshauri.
Aidha Mradi huo umetekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ikiwa ni Tshs. 2,158,984,651.00 na awamu ya pili ni Tshs.1,292,343,850.00, fedha ambazo zinatolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kupitia Mpango wa Uendelezaji wa Miji unaofadhiliwa kwa Mkopo toka Benki ya Dunia.
Mradi huo ulianza tarehe 22/05/2015 na umekamilika tarehe 10/11/2017 . Mradi huo umesimamiwa na Mtaalamu Mshauri GEOMERTY CONSULTANTS LTD wa Dar-es salaam na umejengwa na kampuni ya ujenzi ya CHINA HUNAN CONSTRUCTION ENGINEERING GROUP EAST AFRICA LTD yenye Tawi lake jijini Dar –es Salaam. Hadi sasa Mkandarasi ameishalipwa Tshs, 3,220,995,229.09 sawa na 93 % ya fedha zote na kusalia Tshs, 230,333,271.91 ambazo atalipwa baada ya kukamilisha marekebisho na muda wa matazamio ya mradi.
Aidha Waziri Jaffo ameitaka Halmashauri kuendelea kuwa wabunifu, na kuisimamia kikamilifu stendi hiyo ili kuongeza Mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuwa nia na matokeo ya mradi huo ni kuongeza Mapato kwa Halmashauri pamoja na kutoa huduma kwa wananchi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.