SENDIGA AKOSHWA NA HATUA ZA UJENZI WA MADARASA MANISPAA YA MPANDA
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amepongeza usimamizi wa ujenzi wa miradi ya vyumba vya mdarasa katika shule za Sekondari Lyamba, Mpanda Day na Misunkumilo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Katika ziara yake aliyoifanya leo Oktoba 25,2022 ya kukagua miradi hiyo Queen_Sendiga ametoa wito kwa wasimamizi kuhakikisha wanasimamia vizuri hadi mwisho kama ambavyo miradi imeanza ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na ubora unaostahili.
“Niwapongeze saana viongozi wote ambao mnasimamia miradi hii, nimeridhishwa nah atua za ujenzi Pamoja na namna ujenzi unaovyofanyika, kama mtaendelea hivi ni Imani yangu kwamba miradi hii itakamilika kwa wakati na ubora unaostahili” alisema Sendiga
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Mpanda, Haidary Sumri amemshukuru Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na viongozi wengine kwa namna ambayo wamekuwa wakipita kukagua miradi mara kwa mara jambo linaloongeza umakini wakati wa ujenzi na kusimamia ipasavyo.
Aidha Meya amemuahidi kiongozi huyo kuendelea kusimamia vizuri na kuhakikisha Manispaa ya Mpanda inaendelea kuwa namba moja katika usimamizi wa miradi kama ambavyo imekuwa ikifanya.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.