RAS KATAVI AIPONGEZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MPANDA KWA KUPATA HATI SAFI
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Mrindoko, Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi Bw.Albert Msovero ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kupata hati safi kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo.
Akitoa hotuba katika Baraza maalum la Madiwani la kujadili hoja za Mkaguzi wa nje lililofanyika leo Juni 18, 2025 katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Mpanda, Msovero amesema kuwa, pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wataalamu wa Manispaa ya Mpanda lakini bado wameonesha weledi mkubwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo zilizo pelekea Halmashuri ya Manispaa ya Mpanda kupata Hati safi kwa miaka mitano mfululizo.
“Msitahiki Meya nikupongeze wewe pamoja na Mkurugenzi kwa kupata hati safi isiyo kuwa na mashaka kwa kipindi chote cha uongozi wenu, kwa zaidi ya miaka mitano manispaa ya Mpanda haijawahi kupata hati yenye mashaka; nawapongezeni sana” Amesema Msovero
Msovero ameendelea kuipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali sanjali na usimamizi mzuri wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo yemepelekea Manispaa ya Mpanda na Mkoa kwa ujumla kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
Msovero amesema kuwa, kwa kipindi cha miaka mitano Wilaya ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla umekuwa na mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo baada ya kutengewa bajeti ya fedha zenye thamani ya Tsh Tirioni 1.3 zilizopelekwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya Uchumi na kijamii.
“Waheshimiwa viongozi tunakubaliana kwamba katika kipindi hiki cha miaka mitano ya Rais mama samia mkoa huu wa Katavi umepata mabadiliko makubwa sana, katika kipindi hiki Mkoa wetu umepokea zaidi ta Shilingi Tirioni moja ma milioni mia tatu arobaini na tano ambazo zimekwenda katika sekta mbalimbali katika mkoa wetu wa Katavi”. Amesema Msovero.
Kwa upande wake Msitahiki Meya wa Manispaa Mhe Haidary Sumry amesema kuwa, katika kipindi cha uongozi wake shughuli nyingi na miradi mingi ya kimaendeleo imefanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya kila kata, ujenzi wa shule ya English Medium iliyoko kata ya Misunkumilo, uchongaji wa barabara kwenye kata zote na miradi mingine mingi, yote hayo yamekuwa chachu katika kuwaletea wananchi maendeleo sanjali na upelekaji wa huduma kwa wananchi. Miradi hii imefanyika kwa kutumia fedha za mapato ya ndani na fedha kutoka serikali kuu.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.