WAALIMU WAPIGWA MSASA WA ELIMU JUMUISHI
Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala ndugu Emmanuel Vuri akimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda amewataka Waalimu waliopata mafunzo ya Elimu Jumuishi kutumia elimu waliyoipata katika Semina ya elimu Jumuishi kuwafundisha wanafunzi ili kuongeza ufaulu.
Vuri ameyasema hayo Julai 11/06/2025 katika hafla ya kufunga semina ya Elimu Jumuishi iliyoandaliwa na kuratibiwa na mradi wa Shule Bora na kueleza kuwa Elimu jumuishi ni msingi wa haki, usawa na utu katika jamii.
‘Elimu Jumuishi ni elimu inayomtambua kila mtoto kuwa ana uwezo wa kujifunza, bila kujali tofauti zake za kimwili, kiakili, kijamii au kitabia. Kwa hiyo, mafanikio ya mafunzo haya hayaishii katika ukumbi huu, bali yanaanza hapa. Mafanikio halisi ni pale mtakaporejea katika maeneo yenu na kwenda kuweka katika vitendo yale yote mliyoyajifunza. Alisema Vuri
Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo wakiwakishwa na mwalimu Zuhura Kapama ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nyerere wameeleza kuwa mafunzo yamewapa uelewa wa kina juu ya umuhimu wa kuandaa mazingira jumuishi ya kujifunzia, mbinu shirikishi za ufundishaji, matumizi ya vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, na pia namna bora ya kushirikiana na familia na jamii katika kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma.
Aidha wameahidi kutumia mbinu zote walizofundishwa na kwamba wataenda kutekeleza kwa vitendo falsafa ya elimu jumuishi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.