TANGAZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda anawatangazia wafanyabiashara wote wanaofanya biashara ndani ya Manispaa kulipa ushuru wa huduma (Service Levy), kodi ya mabango, leseni za biashara, leseni za video, kodi ya vibanda vya masoko au stendi kabla ya tarehe 05 Januari 2026.
Pia anawakumbusha wakazi wote kulipa vibali vya ujenzi. Pindi wanapotaka kuanza ujenzi wowote pamoja na kuondoa vibanda vilivyojengwa/kuwekwa maeneo yasiyo rasmi au maeneo ya hifadhi ya barabara, sambamba na kuwahimiza wamiliki wa vyombo vya usafiri wanaosafirisha abiria ndani na nje ya Halmashauri ya Manispaa kufuata utaratibu wa kupakia abiria na kushusha abiria stendi na vituo vinavyoruhusiwa.
Kumbuka kutokulipa kodi/ushuru kwa hiari ni kosa kisheria, hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yako ikiwemo kulipa faini au kushtakiwa mahakamani au vyote kwa pamoja.
Tangazo hili limetolewa leo tarehe 31.12.2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
IJENGE HALMASHAURI YAKO KWA KULIPA USHURU.
FERDINAND JOHN
KAIMU MKURUGENZI
MANISPAA YA MPANDA
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.