CHANJO YA MATONE YA POLIO KUTOLEWA NYUMBA KWA NYUMBA
Mganga mkuu wa mkoa wa katavi Dkt.Omari Sukari amezindua Kampeni ya Utoaji wa Chanjo ya Matone ya POLIO wote walio na umri chini ya miaka mitano. Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo tarehe 18 Mei 2022 itafanyiaka nyumba kwa nyumba inatarajiwa kufanyika kwa siku nne ambao itahitimishwa tarehe 21, mei 2022 ambapo watoto 189,465. Wanatarajiwa kupata chanjo hiyo
Katika Mkoa wa Katavi Kampeni hiyo inatekelezwa katika Wilaya za Mpanda, Mlele, Mpimbwe na Tanganyika ambapo uratibu wa Utoaji wa Matone ya Chanjo ya POLIO umeanza kutekelezwa katika ngazi za Halmashauri zote ndani ya wilaya hizo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi amezindua Kampeni hiyo kwa kushiriki kutoa chanjo ya Matone ya POLIO ambapo ameshiriki kwa kutembelea baadhi ya nyumba na kutoa chanjo kwa watoto chini ya miaka 5 walioko majumbani katika Kata ya Ilembo.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo katika Kituo cha Afya Ilembo kilichopo Manispaa ya Mpanda, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.Omari Sukari ametoa rai kwa Wazazi, Walezi na Wananchi kwa Ujumla kutoa Ushirikiano kwa Timu za Wataalamu zinazopita nyumba kwa nyumba kutoa huduma hiyo ya Matone ya Chanjo ya POLIO.
Amesema lengo la Mkoa ni kuhakikisha kuwa watoto wote wenye Umri chini ya Miaka 5 wanafikiwa na huduma hiyo na kwamba wamejipanga kuhakikisha kuwa maeneo yote yenye watoto kama vile Mashuleni, pamoja na vituo vya Malezi yanafikiwa.
Kwa Upande wao Wazazi na walezi waliojitokeza katika kituo cha Afya Ilembo waliowaleta watoto wao wameishikuru Serikali kwa namna ambavyo imechukua hatua za haraka za kuwakinga watoto dhidi hatari ya Ugonjwa wa POLIO.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.