DAS MPANDA AAGIZA USAFI WA MAZINGIRA KUWA ZOEZI ENDELEVU
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi leo Mei 13 imeendelea na utaratibu wa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ambapo leo timu ya Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda imeungana na wafanyabiashara wa soko la Buzogwe pamoja na vikundi kazi vya Kashulili na Buzogwe kufanya usafi katika soko hilo.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kufanya usafi kaimu Tatibu Tawala Wilaya ya Mpanda Ndugu Keneth Pesambili Simuyemba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ameagiza kuwa, maeneo yoye yenye nyasi ndefu kufikia Jumamosi ijayo yawe yamefyekwa na kuwe hakuna nyasi ndefu zinazoonekana katika mitaa yote ya Manispaa ya Mpanda na kwamba eneo litakalokutwa na nyasi mtendaji wa mtaa/kata pamoja na mmiliki wa eneo hilo watawajibika.
Simuyemba ameendelea kuwakumbusha Wananchi wote ndani ya Manispaa hiyo kuwa, siku ya Jumamosi kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa nne ni muda wa kufanya usafi na hivyo wanapaswa kuzingatia hilo kabla ya kufanya shughuli yoyote.
Ameagiza watendaji wa mitaa, watendaji wa kata na wenyeviti wa mitaa wakiongozwa na Afisa mazingira kuhakikisha wanasimamia kikamilifu zoezi hilo la ufyekaji nyasi ndefu katikati ya mji na siku ya Jumamosi utafanyika ukaguzi na hatua zitachukuliwa kwa eneo litakalokutwa halijafanyiwa usafi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.