Mkuu wa Wilaya ya Mpanda mama Lilian Matinga amefanya mkutano wa hadhara na wafanyabiashara wa soko la buzogwe, Mpanda hotel na Buzogwe mapema leo. Mkutano ulilenga kusikiliza kero na matatizo yaliyopo katika masoko hayo umefanyika katika viwanja vya stendi bajaji.
Mhe. DC amewaeleza kuwa kumekuwa na wizi wa mali za wafanyabishara unaendelea kutokea katika masoko yetu unaopelekea uvunjifu wa amani kutokana na baadhi ya watu kujichukulia hatua mkononi. Amewapiga marufuku wafanyabiashara na Wananchi wote wenye tabia ya kujichukulia hatua mikononi nakuwataka waviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.
“Tabia ya kujichukulia hatua mikononi sio nzuri, ni kinyume na sheria, mkimkamata mtuhumiwa wa wizi msimdhulu, mfikisheni kwenye vyombo vya dola ili vifanye kazi yake” Alisema DC Matinga.
Mkuu wa wilaya aliendelea kuwasihi wafanyabiashara kuishi kama ndugu na kila mmoja kuwa mlinzi wa mali ya mwenzake ili maeneo ya biashara yawe salama muda wote ili kila mmoja kwa nafasi yake aendelee kujitaftia riziki.
Ili kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo ya masoko Mhe. DC amewataka wanaosukuma matoroli na mikokoteni wote sokoni kuanzia tarehe 1, desemba 2018. wawe na umoja wao unatambulika pamoja sale ili waweze kutambulika kiurahisi.
“Kuanzia tarehe 1, Desemba 2018, mtu yoyote atakaye kuwa anazulula sokoni si mteja na hana kazi maalumu atakamatwa kama mzululaji, tunataka masoko nyetu yawe salama muda wote”
Aidha aliwataka wafanyabiashara kuzingatia usafi katika maeneo yao ya biashara na kwamba suala la usafi liwe tabia na si kusubili amri au maagizo kutoka kwa viongozi. Mhe DC aliwataka wafanyabiashara kutamka kauli hii “Usafi ni ustaarabu, unaanza na sisi”. Pia amewaagiza wafanyabiashara wote kusafisha maeneo yote yanayowazunguka mita kumi kila upande ikiwa ni pamoja na kusafisha mitaro iliyopo mbele ya maduka au vibanda vyao. Amewaeleza kuwa amefuta utaratibu wa watumishi wa umma kufanya usafi kwenye masoko kila jumamosi ya mwisho wa mwezi badala yake amewataka wenyeviti wa masoko kuwahamasisha wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika kufanya usafi na kwamba usafi ufanyike kila siku na si kusubili mwisho wa mwezi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.