Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mama Lilian Charles Matinga mapema leo amezindua zoezi la kugawa viatambusho vya Wajasiliamali na Machinga katika Wilaya ya Mpanda vinavyofahamika kwa jina la Vitambuliusho vya Mhe Rais. Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashato iliyopo Manispaa ya Mpanda.
Wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo, Mheshimiwa DC ameieleza hadhara kuwa vitambusho hivyo ni muhimu sana kwa wajasiliamali wadogo kwani vitaondoa changamoto za kimazingira zilizokuwa zikiwakabili wajasiliamali na machinga.
“Naomba wote kwa pamoja tumpongeze sana Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kuendelea kuwapigania wananchi hasa wananchi wanyonge. Aidha nimpongeze kwa ubunifu huu wa aina yake wa kugawa vitambulisho kwa wajasiliamali wadogo na machinga ili kuondoa usumbufu waliokuwa wanaupata”. Alisema DC Matinga
Mama Matinga aliendelea kuwaasa wote watakao kidhi vigezo vya kupata vitambusho hivyo kuzingatia sheria kanuni na taratibu za nchi yetu kwa kufanya biashara halali.
“Kuwa na kitambusho hiki hakikupi ruhusa ya kufanya biashara haramu kama biashara ya madawa ya kulevya, bangi, gongo na biashara nyingine haramu. Vitambulisho hivi mvitumie kwenye biashara halali”. Alisema DC Matinga
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Ndugu Dedatus Kangu amewaeleza wajasiliamali na machinga kuwa serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Magufuli imedhamilia kufanya kazi kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu.
“Vitambulisho hivi vinavyoanza kutolewa leo kwa gharama ya shilingi elfu 20 ambayo ni gharama za utengenezaji wa kitambulicho hicho ni kwa ajili ya kuondoa usumbufu waliokuwa wakiupata wajasiliamali na machinga wakati wakifanya biashara zao. Ninakuhakikishia ukiwa na kitambulisho hiki hautopata usumbufu wowote utakapo kuwa unafanya biashara yako, Cha kuzingatia ni kufuta sheria kanuni na miongozo iliyowekwa katika eneo unalofanyia biashara”. Alisema Kangu.
Uzinguzi huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi umekuwa furaha sana kwa wajasiliamali na Machinga. Aidha wananchi wamempongeza Mheshimiwa Rais kwa kitendo hicho cha kuwatambua na kuwapatia kitambulisho ambacho kwa kiasi kikubwa kitapunguza changamoto zao.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.