Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mama Lilian Charles Mtinga mapema leo amefanya mkutano na viongozi wa dini zote. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Mkutano huu unatokana na wimbi la kuibuka kwa nyumba nyingi za ibada katika Wilaya ya Mpanda ambazo inadhaniwa kuwa zimeazishwa bila kufuata sheria na taratibu.
Katika mkutano huu Mhe. DC amewaeleza viiongozi hao kuwa iwapo wanafanya kusanyiko la watu wakati hawana nyaraka zinazo waruhusu kufanya hivyo watakuwa wanafanya kosa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, aidha serikali haito kaa kimya itaanza kuchukuwa hatua mapema ili kudhibiti hilo ambapo viongozi hao wametakiwa kuwasilisha nakala ya za nyaraka zinazowapatia ruhusa ya kufanya makusanyiko kwenya nyumba za ibada.
“Tunazo sheria za kuanzisha nyumba za ibada, na kila kanisa au msikiti unapaswa kufuata sheria hizo kwa kuwa na usajili, hivyo iwapo utaanzisha mkusanyiko wowote bila kuwa na vibali vinayokuruhusu kufanya hivyo utakuwa umekwenda kinyume na sheria za nchi yetu”. Alisema Mama Matinga
Aidha aliwaeleza kuwa, Dini yoyote ambayo itabainika haina nyaraka zinazo ruhusu kufanya hivyo waanze kufunga na kurudi walikotoka kabla serikali haijachukuwa hatua za kisheria.
Mhe. DC ametumia mkutano huo kuwakumbusha viongozi wa dini zote wajibu wao kwa jamii na serikali ikiwa ni pamoja na:-
Pamoja na kuwakumbusha wajibu huo alitoa onyo kali kwa viongozi wa Dini zote ambaopo alisema, “Wale wanaowahubilia watu kuwa wanaponya UKIMWI na kuwakataza waathirika wasitumie dawa waache maramoja” aliendelea kukieleza kikao kuwa kitendo cha kuwahubiria watu na kwakataza kutumia dawa kimesababisha vifo vingi na hivyo kuisababishia harasa serikali kwa kupoteza nguvu kazi
Mhe. DC aliendelea kukemea vikali tabia ya kuseng’enya madhehebu mengine na viongozi wa madhehebu au misikiti. Kitendo hicho cha kusengenya na kuponda ni kitendo kibaya ambacho kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani. Aidha aliwasisitiza kuwa badala ya kusengenya au kuponda wawakumbushe wananchi juu ya kufanya kazi kwa bidii, kulipa kodi pamoja na kushirikiana na Serikali.
Nao viongozi wa dini walimpongeza Mhe. DC kwa kuwakutanisha na kumuomba utaraibu huo uwe endelevu kwa kuwa unatoa fulsa ya kukumbushana wajibu wa kila dini Nchi yetu.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.