DC MPANDA ASHIRIKI UJEZI WA ZAHANATI YA DILIFU
Katika Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru na 59 ya Jamhuri Disemba 9,2021, Novemba 25,2021 Viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya tanganyika ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Onesmo Buswelu ,Mkurungenzi Mtendaji wa Manispaa Bi.Sophia Kumbuli na Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe.Haidary Sumry wameungana na Wananchi wa Kijiji cha Dilifu Kata ya Magamba katika zoezi la kumwaga jamvi katika Ujenzi wa Zahanati ya Dilifu kwa lengo la kutia chachu na kuhamasisha Wananchi kujitolea.
Kabla ya kuzungumza na Wananchi waliojitokeza,Mkuu wa Wilaya ameshiriki zoezi la kuchanganya zege akiambatana na Viongozi wengine kwa kushirikiana na Wananchi ambapo amewapongeza Wananchi wa Kijiji hicho kwa namna walivyojitokeza na kujitolea nguvu kitendo alichosema inatia Moyo kuona Wananchi wakijitokeza kushiriki Ujenzi wa Miundombinu kwani kujitolea kulizanza enzi za Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Katika kuunga juhudi za Wananchi, Manispaa ya Mpanda imetoa Mifuko 20 ya Saruji huku Mstahiki Meya akichangia Mifuko 5.
Akitoa taarifa ya Ujenzi wa Mradi huo Mganga Mkuu wa Manispaa Dkt.Paul Swakala amesema kukamilika kwa Zahanati hiyo kutapunguza msongamano wa Wagonjwa katika Kituo cha Afya Ilembo,kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya Afya ya Baba,Mama na Mtoto pamoja na kusaidia kupunguza Vifo vya Mama na Watoto wenye Umri chini ya Miaka 5 kwa Wakazi wapatao 9915 wa Kijiji hicho na maeneo ya jirani.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.