DC Mpanda uzindua zoezi la ugawaji wa vitabu vya miongozo ya Elimu.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe Jamila Yusuph amefanya uzinduzi wa ugawaji wa vitabu vya miongozo ya Elimu. Uzinduzi huo umefanyika mapema leo katika kiako cha wadau wa elimu wa Manispaa ya Mpanda kilichofanyika kaitika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.(Mpanda Municipali Social Hall)
Akiongea katika kikao hicho Mhe. Jamila alieleza kuwa, Ili miongozo hii ilete matunda tarajiwa inapaswa kueleweka vizuri na wadau wa elimu wa ngazi zote ikiwemo ngazi ya shule na jamii, aidha Miongozo hii imeanisha masuala mbalimbali yakielimu ikiwamo changamoto na utatuzi wake ili kuboresha utoaji wa elimu ya msingi na sekondari.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ndugu Deodatus C Kangu ikitoa taarifa kwa mgeni rasmi mbele ya wadau wa elimu ameeleza kuwa, Miongozo hii imelenga kuthibiti utoro wa wanafunzi ambao ni kikwazo kikubwa katika ufundishaji na ujifunzaji ambapo Maafisa Watendaji wa Kata/Mitaa wanapaswa kushughulia utoro kwa kutoa Elimu kwa jamii kupitia vikao na nyumba za ibada kuhusu sheria ya elimu na. 25 ya 1978 inayo eleza kuwa anaye sababisha mwanafunzi kutohudhuria shule atafungwa jela miezi 6 au kutoa faini kati ya shilingi 30,000 hadi 50,000.
Mwalimu Mkuu/Mkuu wa shule ahakikishe kuwa a)Wanafunzi wanaitwa majina mara 2 kwa siku. b)Kumwita mzazi shuleni iwapo mtoto wake hata hudhuria shuleni siku 2 mfululizo ili atoe maelezo.
Afisa Elimu Kata kila wiki atapokea majina ya wanafunzi ambao hawakuhudhuria shuleni siku 5 mfululizo na kuyapeleka kwa WEO kwa hatua tajwa hapo juu. WEO atatakiwa kuchukua hatua na kutoa taarifa ya utekelezaji kwa DC, MD na Afisa Tarafa
Aidha muongozo utasaidia kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimu ya msingi. Ili kuimarisha ufundishaji inaelekezwa Kila Kata iwe na Kamati ya Elimu ya Kata (KAEKA). Mhe. Diwani atakuwa M/kiti, AEK katibu, wajumbe ni WEO,VEO,Wenyeviti wa Mitaa, kamati za shule na Walimu wakuu/Wakuu wa shule.
Kamati itafanya kikao cha KAEKA Kila baada ya miezi 3 kinacho tanguliwa na ziara katika shule zote katani Kubainisha changamoto za kielimu na kuzipatia ufumbuzi. Miongoni mwa changamoto hizo zaweza kuwa ni upungufu wa miundombinu, utoro, mdondoko, wanafunzi kutopata chakula cha mchana shuleni, unyanyasaji wa kijinsia.
Muongozo huu utasaidia kuondoa upungufu wa miundombinu ambapo Mkakati unaelekeza kuondoa upungufu wa miundombinu na msongamano darasani kwa kuwatumia wadau na jamii, Inaelekezwa kuwa
1.Kila mwaka jamii inayoizunguka shule kupewa malengo ya ujenzi wa maboma ya vyumba viwili vya madarasa/Utengenezaji thamani
2.Halmashauri kutenga katika bajeti ya maendeleo 10% ya mapato ya ndani kwaajili ya kumalizia miundombinu ya shule kila mwaka
3. UJenzi kuwa moja ya kipimo cha utendaji wa MD, WEO na VEO
Muongozo huu utasaidia kuondoa changamoto ya ukosefu wa chakula ambapo usala la chakula shuleni itakuwa lazima. katika kutekelea jambo hili WEO,VEO na Kamati za shule zitaunda kamati za kusimamia chakula na ziandae mpango shirikishi kuwezesha uchangiaji chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda alihitisha kwa kusema kuwa ili miongozo hii ilete tija tarajiwa inapaswa kuwafikia wadau wote kwa utekelezaji hivyo alielekeza mambo yafuatayo:-
1. Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu kuhakikisha Kamati/Bodi za shule na kwa kipekee walimu wote wanapitishwa katika vipengele vya miongozo ikiwemo utatuzi wa utoro wa walimu.
2. Maafisa Watendaji wa Kata wahakikishe wazazi/jamii inapitishwa katika maeneo ya mwongozo ikiwemo kukomesha utoro na kuchangia maendeleo ya shule.
3. Ofisi zote za kata ziandae vikao vya kuelezea miongozo hii kwenye kata zao.
Baadhi ya wadau wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, wameishukuru serikali kwa kuandaa na kuzindua miongozo itakayosaidia kuinua sekata ya elimu, aidha wameeleza kuwa kwa kuanzisha sula la la chakula shuleni kuwa lazima litasidia watoto wetu kuboresha afya zao pamoja na kupata nafasi ya kujifunza kwa utulivu bil kuwa za njaa.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.