Wakazi wa mkoa wa Katavi wanatakiwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwa kuwapeleka watoto wao wenye umri chini ya miaka 5 kwenye vituo vya Afya, zahanati na maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya kutoa chanjo ya kukinga magojwa ya Surua, Polio na Rubella.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa Mkoa wa Katavi Comrade Juma Z. Homera katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo ofisini kwake. RC Homera elieleza kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau imeandaa kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo za Surua, Rubella na Polio. Kampeni hii yenye kauli mbiu isemayo“Chanjo ni kinga; Kwa pamoja tuwakinge” itafanyika kwa utaratibu wa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano kupewa chanjo.
Aidha alifafanua kuwa lengo mahususi la kampeni hii ya kitaifa ni kuzuia na kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambayo ni ugonjwa wa Surua, Rubela na Polio kwa kutoa chanjo kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 pamoja kuongeza kinga kwa watoto wote kwa kuwapatia chanjo hata kama wameshapata chanjo hizo katika utaratibu wa kawaida wa kutoa huduma za chanjo.Kampeni itafanyika kitaifa kwa siku tano (5) kuanzia Alhamisi tarehe 26 hadi Jumatatu tarehe 30 Septemba,2019 . Siku hizi zitatumika kutoa chanjo kwa watoto wote waliolengwa
RC Homera amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliolengwa wanapata chanjo kwa kuwa Magonjwa ya Surua na Rubella hukingwa kwa chanjo ya Surua-Rubella. “Ni muhimu kwa mzazi kuhakikisha mtoto anakamilisha chanjo zote ikiwemo chanjo ya marudio ya Surua-Rubella ili kuimarisha kinga” Alisema RC Homera. Mtoto anapougua Surua au Rubella apelekwe mapema kituo cha afya kwa matibabu na ushauri. Mtoto mwenye Surua au Rubella apewe vinywaji na chakula cha kutosha. Chanjo hizi ni salama zimathibitishwa na shirika la Afya Duniani na Wizara ya Afya.
“Chanjo hutolewa bila malipo katika vituo vyote vya serikali na watu bianafsi. Utamkinga mtoto wako na maisha yake ya baadae kwa kuhakikisha anakamilisha ratiba ya chanjo .Mtoto asiyekamilisha ratiba ya chanjo ni hatari kwa maisha yake na jamii inayomzunguka kwani ni rahisi kuambukizwa magonjwa na kuambukiza wengine” Alisema RC Homera. Aidha amewatahadharisha wote watakao jaribu kupotosha au kuihujumu serikali kwa kukwamisha kampeni hii kuwa watachukuliwa hatua za kisheria
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.