KATAVI YAPOKEA SH BIL.9.8 MRADI WA BOOST
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amepokea 9.807, 200,000/= kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya elimu msingi (ali maarufu BOOST) katika mkoa wake
Mhe. Mrindoko amesema ujenzi wa miundombinu hiyo utatatua changamoto ya upungufu wa miundombinu katika sekta ya elimu mkoani kwake.
Amebainisha kuwa bil. 5.4 zitajenga shule mpya 10, bil. 3.51 zitajenga madarasa mpya 135, mil. 359 zitajenga vyumba vya madarasa ya mfano ya elimu ya awali 10, mil. 206.8 zitajenga matundu ya vyoo 94 na mil. 100 zitakarabati shule za msingi kongwe 2 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Ameongeza kuwa kiasi kingine cha fedha hizo kitajenga nyumba 2 za walimu katika Wilaya ya Mlele na Tanganyika, zitatumika kununua madawati, meza na viti kwa ajili ya wanafunzi na walimu na kujenga vichomea taka katika shule na ofisi za walimu.
Mhe. Mrindoko ameelekeza kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo unatakiwa kuzingatia thamani ya fedha katika kila mradi; mfano kama ni ujenzi wa vyumba vya madarasa au utengenezaji wa samani (madawati na meza) lazima thamani yake ionekane.
Amesema mkoa wake utafuatilia ujenzi huo ili kuhakikisha fedha zimetumika kwa ufanisi, utaratibu na malengo yaliyokusudiwa bila chenga, bila kubadilisha matumizi wala kufanya ubadhirifu wa fedha hizo.
Mhe. Mrindoko amewahimiza wasaidizi wake kufanya maandalizi na kuhakikisha kuwa ujenzi wa miundombinu ya elimu msingi katika mkoa wake unakamilika kabla Juni 30,2023. Ujenzi huo unatakiwa kuanza mara moja kuanzia sasa.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.