Wakazi wa Kata ya Nsemulwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameanza kupata huduma ya upasuaji kwa wakina mama wajawazito ambapo walikuwa wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Akizungumza baada ya kufanya zoezi la uzinduzi wa huduma hiyo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Daktari Paul Swakala ameeleza tayari halmashauri imekamilisha huduma hiyo kwa vituo vyote sita (06) ili kuwarahisisha waananchi kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali.
Amesema kuelekea huduma ya bima ya afya kwa wote Halmashauri imejipanga kuweka miundombinu bora ya utoaji wa huduma za afya Ili ujio wa huduma ya bima ya afya kwa wote itakapokamikia wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.
Amesisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia miongozo ya wizara ya afya kwa wahudumu kutoa huduma stahiki kwa wananchi ili kuepusha malalamiko.
Kwa Upande wao Wananchi wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwatatulia Changamoto ya Hiyo ambapo walikuwa wanalazimika kutembea muda mrefu kufata huduma hiyo.
Pia wameipongeza ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kwa kuweza kusimia na kukamilisha ujenzi na utolewaji wa huduma ya Upasuaji katika kituo hicho cha Afya (Nsemulwa Health Centre), Hatua ambayo itapunguza vifo vya Mama na Mtoto kwa Kiasi kikubwa
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.