Kumekua na taarifa inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo chanzo chake ni chombo cha habari cha ‘Azam TV’ inayosema….
‘Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imeshindwa kufika lengo la ukusanyaji wa mapato. Yafanikiwa kukusanya shilingi bilioni moja kinyume na malengo waliojiwekea ya shilingi bilioni 27.4 katika kipindi cha bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018’
Taarifa hiyo sio ya kweli, ninawaomba umma kwa ujumla waipuuze, kwakuwa haina hata chembe ya ukweli ndani yake.
Ukweli ni kwamba Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ilikisia kukusanya kiasi cha bilioni 27.46, kati yake bilioni 2.37 ni kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani, bilioni 17.32 ni ruzuku kutoka serikali kuu na bilioni 7.77 ni michango ya wafadhili mbalimbali.
Aidha hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2017 Halmashauri ilikwishakusanya shilingi bilioni 1.04 kati ya bilioni 2.37 ambayo ni sawa asilimia 45 ya makusanyo kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Kutokana na upotoshaji huo, ofisi ya Mkurugenzi inakitaka chombo cha habari cha Azam TV kukanusha taarifa hiyo ndani ya saa 48 kuanzia tarehe ya leo. Isipotekeleza hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya chombo hicho.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.