Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. William Luvuvi amefanya mkutano wa hadhara na wakazi wa Manispaa ya Mpanda mapema leo katika viwanja wa Azimio.
Katika mkutano huo uliosheheni umati mkuwa wa watu, Mhe. Waziri amesikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zinazohusiana na ardhi. Pia Mhe. Waziri amewataka viongozi wote wa idara ya ardhi kuwa waadilifu ili kuepuka migogoro ya ardhi.
Aidha mhe. Lukuvi ametoa onyo kali kwa maafisa ardhi watakao sababisha migogoro ya ardhi kuwa watafukuzwa kazi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Waziri amewaeleza wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano imedhamilia kutatua migogoro ya ardhi.
“Ndugu wananchi wa Mkoa wa katavi niwaeleze tuu jambo moja, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, imedhamilia kutatua migogoro ya wananchi, na mimi Waziri nimetumwa na mhe. Rais kuhakikisha migogoro yote ya ardhi inatatuliwa” Alisema Lukuvi.
Katika mkutano huo mhe. Waziri amewataka viongozi kuto kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na badala yake viongozi wametakiwa kuwafuata wanchi katika maeneo yao ili kutatua kero na matatizo mbalimbali zinazo wakabili wananchi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.