Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu Charles Francis Kabeheo mapema leo amezingua vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa katika shule ya msingi Nyerere iliyo kata ya kawajense katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Ujenzi wa vyumba hivyo bora na vya kisasa zaidi vyenye umeme, samani nzuri, vioo vya kisasa, na marumaru vitasaidia kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi madarasani.
Shule ya msingi Nyerere ipo umbali wa kilomita 06 kutoka Mpanda Mjini. Ni Shule ya kutwa kwa Watoto wa kawaida na wale wenye Mahitaji Maalum. Shule ina vyumba vya Madarasa 08 na Jumla ya wanafunzi 3,022 ambao ni kuanzia darasa la awali Mpaka Darasa la saba hivyo kufanya uwiano wa vyumba vya madarasa na Wanafunzi kuwa 1:378. Vyumba 03 vya Madarsa vinavyozinduliwa leo vinaifanya Shule kuwa na vyumba vya Madarasa 11 hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa vyumba vya Madarasa.
Ujenzi wa vyumba 03 vya Madarasa mpaka unakamilika umegharimu Tshs 42,244,400.00 kati ya fedha hizo Wananchi wamechangia Tshs 6,192,500.00, Halmashauri Tshs 16,551,900.00 na Serikali kuu kupitia EP4R Tshs 19,500,000.00.
Aidha kiongozi wa mbio za mwenge amewataka waalimu na wanafunzi kuwa waangalifu na kutuvitunza vyumba hivyo pamoja na samani zilizomo.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.