“Sisi kama madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda tunakupongeza sana Mkurugenzi pamoja na timu yako kwa uzalendo wa kusimamia madarasa haya ambayo yamejengwa kwa kiwango kizuri kwa fedha kidogo.” Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispa ya Mpanda ndugu Philip Mbogo wametoa pongezi hizo wakati wa ukaguzi wa vyumba viwili vya madarasa vya shule ya sekondari ya Misunkumilo vilivyo jengwa kwa gharama ya Tsh. 37,108,000.
Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa ziara ya madiwani ya kukagua miradi iliyo tekelezwa kama utaratibu walijiwekea wa kutembelea miradi kabla ya kufanya mkuutano wa robo ya nne wa baraza la madiwani.
Aidha wakati wa ziara hiyo madiwani walifanikiwa kutembelea eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kakese ambayo inajengwa kwa ushirikiano wa serikali na wananchi amabapo michango ya wananchi katika ujenzi wa shule hiyo hairidhishi na hivyo Wamemtaka mkurugenzi na diwani wa kata ya kakese kuwahamasisha wananchi kuchangia ili Januari mwaka 2019 shule hiyo ianze haraka.
Katika ziara hiyo madiwani waliweza kutembele mradi wa skimu ya umwagiliaji wa Kakese – Mwamkulu, Zahanati ya Kakese na zahanati ya Mlima Kipala ambapo walimuomba mkurugenzi apeleke wataalam haraka ili zahanati ya Mwamkulu ianze kuwasaidia wananchi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.