Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imefanya mkutano wa wadau wa elimu tarehe 03/04/2018. Mkutano huu unajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo wanafunzi wenyewe, walimu, wazazi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Walimu Wakuu, Wakuu wa shule, Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Vituo vya Walimu (Klasta), TAHOSSA, Viongozi wa CWT, Katibu TSC Wilaya, Wathibiti ubora wa shule, Maafisa Elimu Wilaya, madiwani, pamoja na mheshimiwa Mkuu wa Wilaya. Aidha mkutano huu inahusisha viongozi wa dini, viongozi wa siasa, taasisi za kiraia na wafadhili mbalimbali wa elimu na wadau wengine.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika kikao hiki aliipongeza Manispaa ya Mpanda kwa kuitisha kikao hiki muhimu na kuwaomba viongozi na wadau wote wa elimu kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufaulu na hatimaye mkoa kurudi katika nafasi ya kwanza kitaifa.
Aidha mgeni rasmi aliwataka wazazi na jamii nzima kuzingatia na kuutafasili vizuri waraka wa elimu bure ili kila mmoja atimize wajibu wake. Alisisitiza kuchangia chakula mashuleni na mambo mengine yanayoamuliwa na bodi za shule ili wananfunzi wasome katika mazingiara mazuri ili waweze kufauru kwa alama za juu.
Mkutano huu huitishwa kwa malengo mahususi ya Kutathmini mafanikio ya mfumo shirikikishi wa ufuatiliaji elimu na tathmini katika elimu, Kutathmini vikao vya wadau wa Elimu vya mwaka 2017 ngazi ya kata na mitaa na mkoa kwa ujumla, Kutathimini matokeo ya Mitihani ya Kitaifa ya mwaka 2013,2014,2015, ,2016 na 2017 kwa Manispaa ya Mpanda na mkoa kwa ujumla, Kuwapatia taarifa mbalimbali wadau wa Elimu wa Manispaa ya Mpanda na mkoa kwa ujumla ili kuwaongezea kasi ya utendaji na hivyo kuendeleza mafanikio tuliyoyapata katika Halmashauri na Mkoa wetu;
Aidha kikao hiki kina lengo la Kuongeza umoja, ushirikiano na upendo baina ya wadau wa elimu na viongozi wa Elimu katika Manispaa ya Mpanda na mkoa kwa ujumla kwa lengo la kuongeza ufanisi katika elimu.
Aidha kulifanyika majadiliano ya uwajibikaji yaliyohusisha wadau wote yalifanyika ili kuboresha sekta ya elimu katika Manispaa ya Mpanda na mkoa kwa ujumla, ambapo kwa kauli moja wadau wote waliazimia kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano na ufanisi ili kuinua kiwango cha elimu.
Sambamba na hilo, Mkurugenzi wa wa Manispaa ya Mpanda alitoa taarifa ya mpango na mkakati waliojiwekea ili kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa mwaka 2018 katika madarasa ya awali hadi darasa la saba. Halimashauri imejipanda kuongeza kiwango cha ufaulu kwa darasa la saba kutoka asilimia 90.01 mwaka 2017 hadi asilimia 99 mwaka 2018 na darasa la nne kutoka asilimia 92.48 mwaka 2017 hadi asilimia 99 mwaka 2018.
Kikao hicho kilihitimishwa kwa zawadi zilizo andaliwa na ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya mpanda kwenda kwa waalimu, wanafunzi, wazazi na wadau waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2017 ambazo zilikabidhiwa na mgeni rasmi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.