MANISPAA YA MPANDA YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUPATA HATI SAFI
Kamati ya fedha na utawala ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo na kuoneshwa kuridhishwa na maendeleo yake.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mhe. Haidary Sumry, imekagua mradi wa ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ya hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambapo ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikia huku akimpongeza Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt Paul Swakala kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.
Nao wajumbe wa kamati hiyo William Mbogo (Diwani wa kata ya Majengo) na Chrisant Mwanawima (Diwani wa kata ya Kasokolo) wamesema kwa hatua mradi huo ulipofikia ni wazi kuwa umetekelezwa kizalendo na kuonesha thamani ya fedha.
M…
[15:21, 6/21/2023] DON MUSIC SOUND: MANISPAA YA MPANDA YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUPATA HATI SAFI.
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imepongezwa kwa kupata hati safi katika taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani lililokutana kwa ajili ya kujadili hoja zilizotolewa katika taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kilichofanyika leo Juni 14, 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Akiwatubia wajumbe wa Baraza hilo la Madiwani Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Hassan Rugwa ameeleza kuwa Manispaa ya Mpanda kupata hati safi inatokana na ufanisi na ushirikiano wa Madiwani na Wataalamu wa idara mbalimbali.
Amebainisha kuwa ni madiwani ndio wenye jukumu la kuisimamia Halmashauri hivyo hakuna budi kuwapongeza na kuwatia moyo ili waendelee kubuni mikakati zaidi ya kuweza kuisimamia halmashauri ili kuyafikia malengo yaliyowekwa.
Aidha amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto kwenye baadhi ya maeneo ambazo zimewafanya kupokea hoja kadhaa na kuwataka wataalamu wa Manispaa kushirikiana na madiwani ili kufanya hoja hizo kutojitokeza tena kwa kuwa hayo yote yapo ndani ya uwezo wa halmashauri yenyewe.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry ameeleza kuwa hadi Juni 2022 halmashauri hiyo ilikuwa imepokea hoja 55 kutoka kwa CAG ambapo hata hivyo hoja 30 zimeshajibiwa na kubakiza hoja 25 ambazo nazo zinaendelea kufanyiwa kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema kuwa ni faraja kwa halmashauri hiyo kuweza kupata hata safi hali inayoonyesha kuwa kuna kazi kubwa imefanywa kwenye Manispaa ya Mpanda.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.