Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga amekabidhi ofisi kwa ndugu Amos Makalla ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Katavi aliyeteuliwa hivi karibuni.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za Mkoa wa Katavi huku yakishudiwa na wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Katavi, wakuu wa taasisi pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali.
Katika makabidhiano hayo, Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga amemkabidhi mkuu wa mkoa mpya shughuli zote zilizokuwa zinafanywa na mkoa pamoja na hatua zilizofikia. Aidha ndugu Amos Makalla ameipokea taarifa hiyo nakusema kuwa mkuu wa mkoa ni taasisi, hivyo anamuhakikishia Mkuu wa Mkoa mstaafu kuwa ataendeleza jitihada zote alizozifanya na kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata huduma bora.
Aidha Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga amemkabidhi mkuu wa mkoa wa Katavi mifuko 500 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya GBP kama sehemu ya mchango wao wa kuendeleza ujenzi wa uwanja wa mwenge jambo ambalo lilimfurahisha sana ndugu Amos Makalla kwa jitihada za Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga za kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga amemshukuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa heshima kuwa aliyompatia kwa kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi kuanzia mwaka 2016
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.