MENEJIMENTI YAPEWA MAFUNZO, TAARIFA ZA KIJIOGRAFIA KUHUSIKA KATIKA KUWEKA VIPAUMBELE.
Wajumbe wa Menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakiongozwa na Mkurugenzi Bi Sophia Kumbuli leo Julai 6, 2023 wamepata mafunzo ya miongozo ya Utekelezaji wa Mpango Kabambe (Mater Plans) na Mfumo ya Taarifa Kijiografia (Geographical Information Systems (GIS) kutoka ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuzikumbusha mamlaka za serikali za mitaa juu ya umuhimu wa kutumia taarifa za kijiografia na mpango kabambe katika kupanga, kugawa, kugawanya rasilimali fedha, rasilimali watu Pamoja na huduma stahiki za kijamii kama miundombinu ya afya, elimu, maji na barabara kwa wananchi, yametolewa katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda na Afisa Mipangomiji Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. George Joseph Miringay.
Akiwasilisha mada mbalimbali juu ya umuhimu wa kuwa na mpango kabambe na matumizizi ya mfumo wa GIS Bw, Miringay amesema kuwa, Mamlaka za Serikali za mitaa zinapaswa kuachana na mazoea ya kupanga mipango ya maendeleo ya kata, mitaa na vijiji kwa mazoea, badala yake zinatakiwa kutumia taarifa za kijiographia na mpango kapambe ili kuweka vipamumbele katika mipango ya maendeledeo.
Kwa upende wake Mkurugenzi wa Manispaa ya mpanda Bi Sophia Kumbuli kwa niaba ya Menejimenti na watumishi wote wa Manispaa ya Mpanda amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasani kwa kuendelea kuleta fedha za maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na kwamba Menejimenti itaendelea kusimamia fedha zote zinazoletwa ili ziweze kutumika kama ilivyokusudiwa ili wananchi waweze kupata huduma zote za msingi pamoja na kuwalete wananchi maendeleo.
Aidha Bi Sophia ameishukuru Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kuendelea kuzisimamia kwa ukaribu Mamlaka za Serikali za mitaa na kuanzisha mifumo ambayo itasaidia katika kupanga, na kugawanya rasilimali fedha, rasilimali watu kwa kuzingatia vipaumbele. Bi Sophia amemuhakikishia Bw. George Joseph Miringay Afisa Mipangomiji Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwamba yote aliyoyafundisha na kuelekeza Menejimenti ya Manispaa ya Mpanda imeyachukuwa na itaendelea kuyafanyia kazi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.