Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ngudu William P. Mbogo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Kakese, Misukumilo, Nsemulwa, Shanwe, Kazima na Ilembo. Ziara hiyo yenye lengo la kuzungumzana wananchi pamoja na kusikiliza kero zao ilianza tarehe 05/09/2018 katika kata ya Kakese na Misunkumilo.
Katika mkutano huo Mstahiki Meya amewataka wananchi wa Manispaa ya Mpanda kuepuka migogoro ya ardhi kwa kuto watumia madalali wakati wanapohitaji kununua viwanja. Ameawataka wananchi kumtafuta mmliki wa kiwanja hasa kwa maeneo ambayo yameuzwa mda mrefu uliopita kama Kasimba, Ilembo, Misunkumilo na Kazima. Aidha amewaeleza wananchi kuwa mara wanapo hitaji kununua kiwanja kwa mtu, wafike ofisi ya ardhi ili kujiridhisha kama muhusika ndiye mmiliki halali wa kiwanja hicho na baadae kwenda kwa mwanasheria kwa ajili kuandikiana mikataba. Pia amewata wananchi kuto watumia maafisa wa ardhi ili kuwatafutia viwanja kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwatia taama ya fedha na hivyo kuuziwa viwanja vya watu wengine.
Katika mkutano hiyo Mheshimiwa Mbogo amewapongeza wananchi kwa kujikita katika shughuli za uzalishaji wa mazao ya chakula. Aidha amewaeleza kuwa sambamba na kujihusisha na kilimo cha mazao ya chakula amewataka kujihusisha na kilimo cha mazao ya biashara ili kujiongezea kipato chao.
“Watafiti wa kilimo cha Pamba na Korosho wamethibitisha kwamba ardhi yetu ya Mpanda inastawisha zao la pamba na Korosho, mazao haya yana tija sana, kwa waliojaribu kulima pamba kwa mwaka huu wamepata faida ya wastani wa laki tano hadi milioni nne kwa heka moja” Alisema Mbogo.
Aliendelea kuwaeleza wanachi wa kata hizo kuwa kilimo cha korosho kimekuwa uti wa mgongo kwa wananchi wa mikoa ya kusini kama Mtwala. “zao la korosho huchukua miaka mitatu hadi mitano kaunza kuvuna, aidha unaweza kuvuna zao hilo kwa zaidi ya miaka 60, sambamba na hilo kwa miaka mitatu ya mwanzo katika shamba la korosho unaweza kupanda mazao mengenie kama karanga, mahindi n.k” alisema Mbogo.
Mheshimiwa Meya amewasihi wananchi kujikita katika mazao hayo ya biashara kwa kuwa miaka mitatu si mingi, aidha gharama za utunzaji wa shamaba la korosho si kubwa ukilinganisha na kilimo cha mazao mengine.
Sambamba na kilimo Mheshimiwa Meya amewatahadharisha wananchi juu ya ugojwa wa EBORA. Ameeleza kuwa mkoa wa Katavi una muingiliano mkubwa wa wageni kutoka nchi jirani, hivyo amewataka wananchi kuwa makini na wageni wasiotambulika. Aidha alizitaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo ambazo ni kuwa na homa kali na kutoka damu sehemu zenye matundu kama machoni sikioni na puani kisha akawaeleza kuwa endapo watamuona mwananchi ana dalili hizo wasimguse badala yake watoe taarifa mapema kwenye uongozi wa eneo husika.
Aidha Mheshimiwa Meya alitumia mikutano hiyo kuwaeleza wananchi mipango na miradi mikubwa inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ikiwa ni pamoja na uandaaji wa mpango kabambe uanendelea, ujenzi wa soko Jipya la kisasa litakalo jengwa kata ya kazima mradi unaotarajiwa kuanza mwakani. Ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi mradi unaojengwa kata ya kazima, ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 7.7 pamoja na stendi mpya ya mabasi ilembo inayotarajiwa kuanza kazi tarehe 30 mwezi huu baada ya vibanda na uzio kukamilika.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.