Mkururugezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ndugu Michael F. Nzyungu, mapema leo amefungua mafunzo kwa wakuu wa Idara/vitengo na watendaji wa kata juu ya miongozo ya upelekaji wa fedha za maendeleo (LGDG).
Mafunzo haya yamelenga kuwafundisha na kuwakumbusha washiriki vigezo vya upatikanaji wa fedha.
Katika ufunguzi huo Mkurugenzi amewaeleza washiriki kuwa serikali ina utaribu na vigezo ilivyo jiwekea katika kutoa fedha za maendeleo na fedha za kuendeshea ofisi, hivyo mafunzo haya yataisaidia Halmashauri kuweza kushinda vigezo vyote na hivyo kuiletea Halmashauri ushindi mkubwa utakaopelekea kupewa fedha nyingi kwa ajili ya kuendesha ofisi katika ngazi zote na fedha za kujenga au kukamilisha miundombinu katika maeneo yetu amabyo ni kipamumbele cha jamii.
Wakati akitoa hotuba ya Ufungunzi Mhe. Nzyungu alisema, “Mafunzo haya ni muhimu sana kwa maendeleo ya Manispaa yetu kwa kuwa yanayohusiana na Mfuko wa Ruzuku ya maendeleo ya serikali za mitaa kwa ajili ya mpango wa bajeti ya mwaka 2018/2019 pamoja na kujiandaa na na mchakato wa maandalizi ya upimaji wa mwaka wa kuwezesha kupokea au kupata Ruzuku ya Maendeleo ya Serikali za mitaa”
Wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkururugezi Nzyungu amewakata washiriki wote wa mafunzo hayo kufuatilia kwa umakini mkubwa mambo yote yatakayo fundisha kwa kuwa baada ya mafunzo utafanyika utekelezaji utakao ambatana na upimaji.
Aidha ameeleza kuwa kwa kuwa wakuu wa Idara wote na watendaji wote wameshiriki mafunzo hayo anategemea halmashauri itafauru vigezo vyote pamoja na upimaji utakaofanywa na serikali na hivyo halmashauri kupata fedha za kuendeshea ofisi pamoja fedha za miradi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.