MKURUGENZI MANISPAA ATEKELEZA AGIZO LA RC
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda leo Oktoba 15, 2023 wameshiki zoezi a usafi wa mazingira katika soko la Mpanda hotel ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa mkoa wa Katavi Bi Mwanamvua Mringoko la kuwataka wananchi wote kufanya usafi wa kina katika maneneo ya makazi na maeneo ya biashara. Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi, Mkururgenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi Sophia J kumbuli amewataka wananchi wote kutii agizo la mkuu wa mkoa wa Katavi ili kuipatia hadhi Manispaa ya Mpanda.
“Ukiwa Manispaa, kipaumbele cha kwanza ni usafi, tujitahidi kufanya usafi wa mazingira ili tuipe hadhi manispaa yetu” alisema Sophia Kumbuli
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Mpanda ndugu Keneth Pesambili ambaye alimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Mpanda, ameendelea kusisiiza usafi na utunzaji wa mazingira kuwa sehemu ya maisha ya kila mtanzania na kueleza kuwa ambaye atakaidi au kushindwa kuafanya usafi kwa hiari yake atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwanamvua Mrindoko akiwa kaitika kikao maalum cha tathimini ya usafi wa mazingira, afya na lishe aliwaagiza Wakurugenzi wote kuhakikisha wanasimamia usafi katika maeneo yao ya utawala na kwamba kila Jumamosi itumike kufanya usafi katika maeneo yote ya makazi na biashara.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.