Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda amefanya kikao kazi na viongozi wa Elimu ngazi za shule, kata na Halmashauri leo tarehe 22/03/2018 ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na elimu huku lengo kuu likiwa ni kuinua ubora wa elimu.
Katika kikao hicho Mkuu wa idara ya elimu sekondari aliwakumbusha viongozi wa elimu majukumu yao ya msingi ambayo wanapasa kuyafanya kila siku ikiwa ni pamoja na kuwasimamia na kuwafundisha waalimu walioko chini yao ili nao waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu. Aidha amewataka walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu elimu ngazi ya kata kuhakikisha wanawasimamia waalimu na kuhakikisha maandalio, vipindi, namna ya ufundishaji vinazingatiwa na kusimamiwa kwa ukaribu ili kuongeza ubora wa elimu. Pia amewataka viongozi wa elimu kuwa na tabia ya kukaa pamoja ili kujadili na kutatua changamoto mbalimbali za kielimu zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kutunga mitihani yenye ubora ili kuondoa dhana ya kukariri maswali kwa wanafunzi. Kikao hicho kilihudhiliwa na wakuu wa idara na vitengo ambao walipewa nafasi ya kueleza mambo mbalimbali hasa sheria kanuni na taratibu zinazopaswa kuzingatiwa katika taasisi zao. Badada ya maelezo yenye ufafanuzi wa kina kutoka kwa wakuu wa idara na vitengo ya Mpanda ndugu Michael F. Nzyungu alipata nafasi ya kuongea nakutoa maelekezo kwa viongozi hao.
mkurugenzi wa Manispaa aliwaeleza viongozi hao kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imekua ikishika nafasi ya kwanza kitaifa kwa miaka miwili mfulurizo, aidha kwa mwaka 2017 Halmashauri ilishuka kutoka nafasi ya kwanza hadi nafasi ya tisa kitaifa. Pamoja na kuwa katika nafasi ya kumi bora nafasi hiyo sio nzuri na sio jambo la kujivunia ukilinganisha na nafasi ya kwanza tuliyoipata kwa miaka miwili mfurulizo. Hivyo amewataka viongozi na waalimu wote kufanya kazi kwa bidii ili turudi katika nafasi yetu ya awali.
Aidha ameendelea kuwaomba viongozi kusimamia na kuendelea kushirikana na kamati za shule pamoja na viongozi wa kata ili kuihamasisha jamii juu ya umuhimu wa kujenga miundombinu ya shule kama maboma ili serikali imalizie kupauwa na kufanya usafi wa miundombunu hiyo. Mkurugenzi amewata viongozi hao kuyatekeleza yote waliojadiliana kwa kuwa wao ndio nwawakilishi wake katika taasisi wanazozitumikia, endapo watashindwa kumsaidia kazi hatosita kutengua nafasi walizonazo ili wapewe watu watakao msadia.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.