Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Rafael Muhuga ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani katika mkoa wa Katavi yamefanyika Wilaya ya Tanganyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, kata ya Sibwesa.
Katika sherehe hizo mkuu wa Mkoa amewashukuru wanawake kwa umoja walionao kwa kuunda vikundi mbalimbali vya kijasiliamali ikiwa ni sehemu ya kutekeleza dira ya nchi ya uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo. Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni.. Kuelekea uchumi wa viwanda, tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini.
Mgeni rasmi amewataka wanawake kuongeza juhudi za kujikwamua kwani katika mkoa wa Katavi takwimu zinaonesha asilimia 33 ya wanawake hawajui kusoma na kuandika . Alieleza kuwa takwimu hizo sio nzuri kisha akaitaka jamii nzima ichukue hatua za haraka kwa kuacha mila potofu, kuwakatisha watoto masomo na kuozesha watoto wadogo kwani ndio chanzo kikubwa cha tatizo hilo.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.