Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege leo hii amefanya lziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda. Katika ziara hiyo mhe. Naibu waziri amefanikiwa kutembelea miradi na vikundi mbalimbali na kujionea hatua mbalimbali za utekelezaji wake.
Aidha naibu waziri amefurahishwa sana na hali ya utekelezaji wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ilembo nakuziagiza Halmashauri nyingine ambazo zimepata mradi wa ujenzi wa stendi kufanya ziara ya mafunzo katika stendi ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa dhana ya kujifunza na kuboresha zaidi.
“Nawapongeza sana kwa utekelezaji na usimamizi mzuri na wa mradi huu wa stendi ya mabasi ya kisasa, nimeridhika na utekelezaji wake na kwa hali hii ninawaagiza Halmashauri ya sumbawanga na halashauri nyingine kuutembelea mradi huu ili waweze kujifunza na kupata ramani ya stendi hii.”
Ujenzi mradi huu wa stendi ya mabasi ulianza mwaka 2014 kwa lengo la kuboresha mapato ya ndani ukiwa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (ULGSP) kwa gharama ya Tsh. 3,451,328,501.00
Katika ziara hiyo ameitaka Halmashauri kuwa na mikakati mizuri ya kuiendesha stendi hiyo ya kisasa huku akiishauri Halmashauri kuwa na mapango endelevu wa kuongeza eneo la stendi kwa ajili ya biashara na upanuzi wa stendi hapo baadae.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.