RC KATAVI AMKUMBUKA NYERERE KWA MATENDO YA HURUMA
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa msaada mbalimbali kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na kuenzi miaka 23 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Akiambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mpanda, Mrindoko amemtaja Hayati Mwl. Nyerere kama kiongozi aliyepiga vita maradhi kupitia falsafa yake ya kupambana na maadui wa Taifa ikiwemo Ujinga na umasikini.
"Tangu wakati huo wa Uhuru vita hiyo imeanza ya kupambana na maadui hao na vita hiyo ni endelevu na inaendelea,naweza nikasema ndani ya Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan mapambano yameendelea kuwa makubwa zaidi kwenye maeneo yote matatu"
RC Mrindoko akiwa ameambatana na viongozi kutoka ofisi yake, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Viongozi wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Mpanda pamoja na viongozi wengine wameweza kutembelea wodi kadhaa kuwajulia hali wagonjwa sambamba na kuwapatia baadhi ya mahitaji kama sabuni, sukari, juisi na mafuta ya kupakaa.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.