RC KATAVI ARIDHISHWA NA UJENZI WA MADARASA MPANDA
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko ameridhishwa na hatua za ujenzi wa vyumba 51 vya madarasa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda. Mhe Mrindoko amefanya ziara ya ukaguzi wa vyumba 51 vya madarasa vinavyogharimu bilioni moja (1) na milionini 20 kwa ajili ya maandalizi ya kuwapokea kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.
Mkuu wa mkoa amewataka watumishi wa Umma na wote wenye dhamana ya kusimamia miradi hiyo kuwa waadilifu, na kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa na kwa ubora na viwango vinavyotakiwa.
Rai hiyo imetolewa 10 Novemba 2022 wakati akikagua Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya Rais Samia katika Manispaa ya Mpanda ikiwa ni utekelezaji wa ratiba ya kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Kwa Sasa hivi tunafuatilia ujenzi huu wa madarasa ya Rais Samia ili kuhakikisha kuwa Ujenzi wa Madarasa yanakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa.Maelekezo ya Mhe.Rais ni kukamilisha madarasa haya Tarehe 15 Desemba 2022 lakini sisi Mkoa wa Katavi tunasema tutakamilisha Ujenzi huu Tarehe 07 Desemba 2022 ili ile wiki moja iwe ni ya Waziri wa TAMISEMI kufanya ufuatiliaji na kumkabidhi Mhe.Rais.”Alisema Mkuu wa Mkoa Mrindoko.
Bi.Mrindoko ameipongeza Manispaa ya Mpanda kwa kusimamia vizuri Ujenzi wa madarasa ya Mhe.Rais Samia ambapo amewataka kuongeza jitihada zaidi ili kuhakikisha kuwa Ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa.
“Nyie Manispaa ya Mpanda mnaongoza kwa kuwa na vyumba vingi vya madarasa na mna vyumba 51 kati ya 119 na katika maeneo niliyopitia nimeridhishwa na hatua nzuri ya ujenzi hivyo msibweteke na sifa na badala yake mjipange kuhakikisha kuwa mnakamilisha Ujenzi ndani ya muda uliopangwa”alisema Bi.Mrindoko.
Aidha Bi Mrindoko ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kuchangia nguvu kazi katika Ujenzi wa Madarasa 119 ili Shilingi Milioni Ishirini iliyotolewa kwa kila darasa itosheleze kumaliza ujenzi huo ambapo amewataka Wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa kia darasa ndani kunakuwepo na viti na meza kwa ajili ya Wanafunzi.
Akiwa Manipaa ya Mpanda Mkuu wa Mkoa Bi Mwanamvua Mrindoko amekagua Ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika Shule za Sekondari Lyamba,Rungwa,Shanwe,pamoja na Mpanda.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.