Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mhe. Amos G. Makalla ameongoza kikao cha kusikliza kero ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake ya kusikiliza matatizo ya wananchi mara mbili kwa mwezi. Mhe. Makalla baada ya kuhamia Mkoa wa Katavi aliweka utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi mara mbili kwa mwezi ambapo wananchi watapata fursa ya kuonana ana kwa ana na Mkuu wa mkoa siku ya Jumatatu ya pili ya mwezi na Jumatatu ya mwisho wa mwezi ili kuwasilisha kero zao.
Katika kikao hicho zaidi ya wananchi 65 wamefika na kuwasilishwa kero zao ambapo zaidi ya asilimia 90 ya kero zilizo wasilishwa ni kero za ardhi zinazotokana na madai ya fidia, kunyanganywa kiwanja, kutopewa hati, kupunjwa viwanja baada ya Halmashauri kupima katika maeneo yao pamoja na kiwanja kuuzwa mara mbili.
Aidha Mhe. Makalla amewaagiza viongozi ambao wamepewa nafasi ya kuwahudumia wananchi kuhakikisha wanatatua kero zote za wananchi zilizo wasilishwa katika kikao hicho. Mhe. Makalla ameagiza mkuu wa wilaya na mkurugenzi kufika kwenye mitaa na kuitisha mikutano katika mitaa hiyo ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi hasa kwenye mitaa yenye kero nyingi za ardhi.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.