Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wametoa tamko la pamoja la kumpongeza Meya kwa kuwa mzalendo kwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda. Tamko hilo limetokana na Mhe.. William Philip Mbogo(Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda) kuamua kubadilisha kibali cha ununuzi wa gari la Meya la kutembelea lenye gharama zaidi ya Milioni 145, na kuamuru fedha hizo zitumike kununua gari kubwa la kubebea taka ili Manispaa iendelee kuwa safi mda wote. Tamko hilo limetolewa na waheshimiwa madiwani katika mkutano wa Barala za Madiwani uliofanyika tarehe 31/10/2017 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.