TCB YATOA BANDARI 15 ZA BATI MANISPAA YA MPANDA
Benki ya biashara ya Tanzania (TCB –Tanzania Commercial Bank) tawi la Mpanda mkoani Katavi imetoa bandari 15 za bati kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zenye thamani ya shilingi milioni kumi tano na laki nne( 15,400,000/=) kwa ajili ya umaliziaji wa vyumba 2 vya madara katika shule ya msingi katavi iliyopo Kata ya Makanyagio.
Akikabidhi mabati hayo kwa mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa katavi Dkt. Baganda Egdius ambaye ni afisa elimu wa mkoa wa Katavi, Meneja wa TCB tawi la Mpanda ndugu Julius Mlang’a amesema TCB kutoa mabati hayo ni kuendeleza sera ya benki anayosema “Elimu ni sera yetu”. Aidha meneja wa TCB aliendelea kueleza kuwa TCB itaendelea kuunga jitihada za Serikali za kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu katika mazingira rafiki.
Diwani wa Kata ya Makanyagio Mhe. Haidary Sumry ambaye ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa niaba ya Halmashauri ameshukuru Benki ya TCB kwa kuweza kutoa bandari 15 za bati kwa ajili ya kusaidia ukamilishaji wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya msingi Katavi.
Mheshimiwa Sumry aliendelea kueleza kuwa changamoto za vyumba vya madarasa na miundombinu mingine katika shule za Manispaa ya Mpanda bado zipo hivyo ameziomba taasisi nyingine na wadau mbalimbali kuendelea kuejitokeza kusaidia ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ili watoto wa kitanzania waweze kupata elimu katika mazingira rafiki.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.