SHULE YA MSINGI KIVUKONI YAMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA
Uongozi na wanafunzi wa shule ya msingi Kivukoni Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imemuomba Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kuwafikishia barua ya shukrani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaondolea adha ya msongamano wa wanafunzi katika Kata hiyo baada ya kutoa fedha kwa ajili ya kujenga vyumba 6 vya madarasa, matundu ya vyoo matatu na madwati 90.
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa mkoa wanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo wamemshukuru Rais kwa kuwajengea miundombinu mizuri ya madarasa na wamemuahidi kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mtihani yao hususani mtihani wa kuvuka darasa la tano unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akitoa taarifa ya shule hiyo kwa mkuu wa mkoa alipofika kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba hivyo, mkuu wa shule ya msingi Kivukoni Mwl. Lucy Msafiri amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 2050 ambapo kabla ya ujenzi wa vyumba hivyo wanafunzi walikuwa wanapata shida kujisomea kwani vyumba vilivyokuwepo vilikuwa
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.