WATUMISHI MANISPAA YA MPANDA WAMUAGA NA KUMKARIBISHA MKUU WA IDARA YA UTUMISHI
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wametumia usiku wa Julai 8, 2025 kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala ndugu Deodatus Kangu ambaye amehamia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni sambamba na kumkaribisha ndugu Emmanuel Vuli ambaye kwa sasa ndiye mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Mpanda.
Katika hafla hiyo watumishi wametumia muda huo kumtakia kila heri sambamba na kumshukuru kwa utumishi wake akiwa Manispaa ya Mpanda kwa zaidi ya miaka 7.
Kwa upande wake Muagwa ndugu Deodatus Kangu ametumia nafasi hiyo kwanza kumshukuru Mungu kwa kwa kumpa kibali cha kutumika katika Manispaa ya Mpanda kwa miaka 7.
" Kwanza kabisa naomba nimshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kutumika hapa kwa miaka 7, nilikuja nikiwa kijana na sasa ni mtu mzima, namshukuru mama (Mkurugenzi), Wakuu wa Idara na watumishi wenzangu kwa upendo na ushirikiano mlionipatia kwa kipindi chote nikiwa hapa, ninaindoka nikiwa nimelelewa na mama na bahati nzuri tena kule Manyoni ninepokelewa na mama" alisema Kangu.
Kwa upande wake ndugu Emmanuel Vuli ambaye ni mkuu wa Idara kwa sasa amewaomba watumishi wote kumpatia ushirikiano kwa kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo ili kumsaidia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
" Ndugu watumishi wenzangu ninaomba ushirikiano wenu, sina ndugu hapa Mpanda, ndugu zangu ni nyie watumishi wenzangu, ninaomba tushirikiane kufanya kazi kwa kufuata sheria kanuni na miongozo ili tuwahudumie wananchi na hivyo kumsaidia Mhe. Rais kazi aliyotutuma" Alisema Vuli
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ametumia nafasi hiyo kumtakia Deodatus kila lililojema na kwamba kwa uwezo wake katika utumishi hamuoni hapo Manyoni anamuona akifika mbali na juu zaidi.
Aidha bi Kumbuli amemkaribisha Ndugu vuli na kueleza kwamba kwa siku chache sana alizofanya kazi na Emmanuel Vuli ameona uwezo wake mkubwa, hivyo Kangu aliyehama ni jembe na aliyehamia ni jembe pia na kwamba kubwa zaidi ni kumpatia ushirikiano.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.